Ndg.Iddy White Mwinuka ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Makambako(MAKUWASA) aliyeteuliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mnamo Semtemba 1,2016 kwa mujibu wa sheria ya maji ya mwaka 2009.
Kabla ya hapo alikuwa mjumbe wa Bodi hiyo miaka sita (6) iliyopita.Pia amewahi kushika nyazifa mbali mbali katika jamii kwa vipindi tofauti tofauti kama vile,Mjumbe wa bodi ya sekondari ya Wanging’ombe kwa muda wa miaka nane,Deo Sanga sekondari miaka mine,Kipagamo sekondari miaka nane,Katibu wa TCCIA wilaya ya Njombe ,Meneja wa Makambako SACCOS kwa muda wa miaka sita.
Mh.Iddy White Mwinuka alizaliwa mwaka 1961 katika kituo cha afya cha Kipengere kata ya Kipengere wilaya ya Wanging’ombe Mkoa wa Njombe,Mh.Mwenyekiti amepata elimu mbali mbali katika shule mbali mbali ikiwemo shule ya msingi kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1978 katika shule ya msingi Kipengere ,elimu ya seondari kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1982 katika shule ya sekondari Njombe ,elimu ya juu kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985 katika sekondari ya Ndanda Mtwara. Mwaka 1985 hadi mwaka 1986 mwenyekiti alijiunga na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka 1987 hadi 1994 mwenyekiti aliajiriwa na kiwanda cha karatasi Mufindi cha Southern paper Mills (SPM) katika idara ya Manunuzi,akiwa kazini alifanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya ngazi ya cheti hadi kufikia stashahada ya ugavi kuanzia mwaka 1991 hadi 1994.Baada ya hapo kwa hiari yake aliamua kuacha kazi na kuendelea na ajira binafsi ambayo mpaka sasa anajishughulisha na biashara ya vifaa vya ujenzi (Hardware) akiwa katika shughuli hiyo aliendelea kuongoza na kusimamia shughuli za kijamii kama vile uenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Makambako,Mjumbe wa bodi ya shule Wanging’ombe na Ukatibu wa TCCIA Wilaya ya Njombe.
Makambako
Anuani ya posta: P.O.Box 940 Makambako
Simu: +255 262730407
Simu ya kiganjani: 08000750041
Baruapepe za Watumishi: md@makuwa.go.tz
Copyright ©2018 Makuwasa . All rights reserved.